Monday, August 4, 2008


Mrisho in New York City July 2008

4 comments:

Anonymous said...

KUFUNGUA MIKATABA.

1.Awamu inayo kuja,kuna mya-nya ya kuziba,
Na hasa inayovuja,itupayo misalaba,
Nchi imekosa tija,sababu ya mikataba,
Kufungua mikataba,na kufunga yenye tija.

2.Kote kunako machimbo,kugemishwa ni msiba,
Kwamba hatuna mitambo,ya kuchimbua miraba,
Wachimbaji toka ng’ambo,bilashaka wanaiba,
Kufungua mikataba,na kufunga yenye tija.

3.Maeneo ya madini,Mwalimu Nyerere Baba,
Alitunza kwa makini,vizazi vije kushiba,
Leo bure masikini,Makaburu wanabeba,
Kufungua mikataba,na kufunga yenye tija.

4.Zinakwenda zinalia,Dhahabu hulia toba,
Lau zingajikalia,aridhini kwenye miba,
Madongo yakalalia,chini zikajisiliba,
Kufungua mikataba,na kufunga yenye tija.

5.Tunafanya biashara,kwa mdogo mrahaba,
Si faida ni khasara,hatutunishi mikoba,
Yahitajika busara,kung’oa hizi ghiliba,
Kufungua mikataba,na kufunga yenye tija.

Anonymous said...

(A).WAWEKEZAJI SI WEZI.
1.Mkapa katukumbusha,Wawekezaji si wezi,
Nchi wanaboresha,kwenye uchumi na kazi,
Wivu unatukondesha,il-hali si malezi !
Wawekezaji si wezi,vigumu kujiridhisha.

2.Mola hajatupofusha,kushindwa kuona wazi,
Nchi wanavyo-ichosha,kwa kuinyonya mizizi,
Ninadhani inatosha,kuwaita majambazi,
Wawekezaji si wezi,vigumu kujiridhisha.

3.Madini wanajitwisha,tena jozi kwa ma-jozi,
Mno wanatu-dunisha,kuinuka hatuwezi,
Aridhini yakiisha,warithi nini vizazi?
Wawekezaji si wezi,vigumu kujiridhisha.

4.Tungejua tungekesha,kwa vilio na machozi,
Kwa lengo kuwahamisha,waondoke walowezi,
Huku wanatuzamisha,wao wanapiga mbizi,
Wawekezaji si wezi,vigumu kijiridhisha.
(B). KUNG’AMUA FUMBO.
5.Kila ukiwatazama, Wazungu kutoka ng’ambo,
Ungedhani watu wema,wapo kunyosha mambo,
Kumbe bila huruma,wana tufumbia fumbo,
Kuja kung’amua fumbo,katikati ya mrama.

6.Wamenyonya tangu zama,wakitugawa majimbo,
Afrika yote nzima,ikawa yao machimbo,
Kuzinduka wakahama,tulipokataa shombo,
Kuja kung’amua fumbo,katikati ya mrama.

7.Kurejea hima hima,na ndoano yenye chambo,
Mikopo yenye gharama,misaada kwenye vyombo,
Lengo lao ni kuchuma,kutuachia makombo,
Kuja kung’amua fumbo,katikati ya mrama.

Omary K.A Msangi,*(KIKORE)
Mkunguni / Sikukuu, Kariakoo
Dar es salaam.

Anonymous said...

NAKUHOJI SERIKALI.

1.Hivi lini serikali,utahamia Dodoma?
Kwako tatizo ni mbali,ama kuna Trakoma?
Kuna nini kule mahali,wendapo wapata homa?
Vipi huendi Dodoma,nakuhoji Serikali.

2.Siewe ulie fasili,kwamba “Dar”unahama?
Dodoma hujawasili,hivi wapi umekwama?
Tujuze jibu kamili,vipi mbona hujasema?
Vipi huendi Dododoma,nakuhoji serikali.

3.Ama tatizo shughuli,kule hutotenda vema?
Vipi hutupi kauli,utuweke palo pema?
Kama tatizo nauli,vipi mbona huja sema?
Vipi huendi Dodoma,nakuhoji serikali.

4.Kwa nini kwa jambo hili,walala unakoroma?
Sijaziona dalili,ama kwenda umegoma?
Dodoma kuna “Mbigili”,ukenda zitakuchoma?
Vipi huendi Dodoma,nakuhoji serikali.

5.Mawazo hujabadili,ama umerudi nyuma?
Dodoma mji dhalili,ama hauna huduma?
Kwako hapastahili,kwa tufaa sisi viuma?
Vipi huendi Dodoma,nakuhoji serikali.

6.Hapa tuache kejeli,hustahili lawama?
Shida ipi ya ukweli,iwe imekuandama?
Ama kuna matapeli,na mji sio salama?
Vipi huendi Dodoma,tatizo ni “TRAKOMA”?

Anonymous said...

NGUVU YA MTU CHUMO

1.Nguvu ya mtu ni chumo,hata kama si msomi,
Hadhi yake ni ngurumo,ifikayo hadi rumi,
Ikikutana na shimo,bila shaka haizami,
Hatakama si msomi,Uraisi Mwenye chumo

2.Kila panapo mvumo,pana riba ya uchumi,
Ndipo penye mu-egemo,kama njia ni ya lami,
Pakikita msimamo,kingine hakisimami,
Hatakama si msomi, Uraisi Mwenye chumo.

3.Leo ni huo mfumo,masikini hatuvumi,
Siasa za mikingamo,na hata za nyumba kumi,
Viongozi waliomo,bila senti hawakemi,
Hatakama si msomi, Uraisi Mwenye chumo.

Omary.K.A Msangi KIKORE,
Management services
T.P.A
HQ.